Soma Biblia Kila Siku 8Mfano
Maneno ya agano yamerudiwa sasa ili kizazi kipya kiingie katika agano alilolifanya Mungu na watu wake (m.10-13:Leo mmesimama nyote mbele za Bwana, Mungu wenu...ili uingie katika agano la Bwana, Mungu wako, na kiapo chake, afanyacho nawe Bwana, Mungu wako, hivi leo; apate kukuweka leo uwe taifa kwake naye apate kuwa Mungu kwako, kama alivyokuambia, na kama alivyowaapia baba zako, Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo). Lakini mpaka leo BWANA hakuwapa moyo wa kujua, wala macho ya kuona, wala masikio ya kusikia, hata leo hivi (m.4). Yaani hawajaelewa mioyoni mwao neema ya Mungu katika kutaka kushirikiana nao. Mtume Paulo anakariri maneno hayo akieleza habari ya ugumu wa mioyo ya Wayahudi walio wengi (Rum 11:8: Kama ilivyoandikwa, Mungu aliwapa roho ya usingizi, macho hata wasione, na masikio hata wasisikie, hata siku hii ya leo). Ugumu huo umetokana na kutolipokea Neno kwa moyo wa ukunjufu (zingatia pia Rum 9:30-32: Watu wa Mataifa, wasioifuata haki, walipata haki; lakini ni ile haki iliyo ya imani; bali Israeli wakiifuata sheria ya haki hawakuifikilia ile sheria. Kwa sababu gani? Kwa sababu hawakuifuata kwa njia ya imani, bali kana kwamba kwa njia ya matendo. Wakajikwaa juu ya jiwe lile likwazalo ambalo ni Kristo Yesu).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 8 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku hasa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Kumbukumbu la Torati, na Yohana pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz