Soma Biblia Kila Siku 8Mfano
Habari ya kahaba ni hali halisi. Pia ni mfano wa dhambi yoyote ile na matokeo yake. Mtu akijisogeza kwake, hila ya kishetani itampofusha hata asiweze kuiona njia ya uzima, wala hajui anateremkia mautini. Huku ukivunja uhusiano mzuri na Mungu, matokeo ya uhusiano na kahaba ni pamoja na kupoteza mali, heshima na miaka ya kuishi. Mwishoni utaomboleza tu kuzimu. Sikiliza, basi, maonyo kama ilivyo katika somo hili. Ikimbie zinaa! Kumbuka pia maombi. Ni msaada mkubwa kwenye njia ya ushindi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 8 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku hasa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Kumbukumbu la Torati, na Yohana pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz