Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 8Mfano

Soma Biblia Kila Siku 8

SIKU 21 YA 31

Sura ya 18 na 19 zinatueleza habari ya mateso na kifo cha Yesu Kristo. Katika somo la leo twahitaji kutambua hiariya Yesu katika kwenda njia ya msalaba! Je! kikombe alichonipa Baba, mimi nisikinywee?(m.11). Kikombe alichompa Baba ni mateso na kifo. Maombi ya Yesu katika bustani iitwayo Gethsemane yanaonyesha hiyo: Yesu akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe(Mt 26:39). Yuda alikuja na kikosi chenye nguvu ya kutosha, lakini Yesu alipojitambulisha wakakutana na nguvu ya kimungu. Wakaogopa na kuanguka chini. Yesu angeweza kuwashinda, lakini akajitoa kwa hiari(m.7-8: Yesualipowaambia, Ni mimi, walirudi nyuma, wakaanguka chini. Basi akawauliza tena, Mnamtafuta nani? Wakasema, Yesu Mnazareti. Yesu akajibu, Nimekwisha kuwaambieni ya kwamba ni mimi; basi ikiwa mnanitafuta mimi, waacheni hawa waende zao)!

siku 20siku 22

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 8

Soma Biblia Kila Siku 8 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku hasa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Kumbukumbu la Torati, na Yohana pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz