Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 8Mfano

Soma Biblia Kila Siku 8

SIKU 26 YA 31

Kwenye msalaba juu ya kichwa cha Yesu paliandikwa: YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI. Ni maneno ya kweli! Utukufu wa Yesu si nguo, maana nguo zake walizichukua (m.23:Askari walipomsulibisha Yesu, waliyatwaa mavazi yake). Utukufu wake ni taji ya miiba na damu (19:5: Ndipo Yesu alipotoka nje, naye amevaa ile taji ya miiba, na lile vazi la zambarau. Pilato akawaambia, Tazama, mtu huyu!). Je, hayo kweli ni utukufu? Ndiyo! Maana alikubali hayo yote kwa hiari, na kwa upendo mkuu. Wanadamu ndio tumestahili hukumu kama hii kwa sababu ya dhambi zetu! Lakini Yesu alikufa badala yetu!Je, umemtukuza Yesu kwa hayo? Unaweza kutumia sifa katika Ufu 5:9-10: Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa, ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.

siku 25siku 27

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 8

Soma Biblia Kila Siku 8 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku hasa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Kumbukumbu la Torati, na Yohana pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz