Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 8Mfano

Soma Biblia Kila Siku 8

SIKU 30 YA 31

Yesu alikwisha waambia wanafunzi wake kwamba baada ya kuuawa atafufuka siku ya tatu (k.m. Mt 12:40: Kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi. Na Mt 16:21: Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka). Lakini kati ya maneno yote ya Yesu, neno hilo ndilo lilikuwa gumu zaidi kwao kuamini! Kwa maana walikuwa hawajalifahamu bado andiko, ya kwamba imempasa kufufuka (m. 9). Lakini baadaye wakaelewa na kuhubiri kwamba hata tukio hilo limetabiriwa na manabii (k.m. 1 Kor 15:4: Alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko)! Kama neno la ufufuo lilionekana ni kweli, je, tuna sababu yoyote kuwa na mashaka juu ya maneno yake mengine?

siku 29siku 31

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 8

Soma Biblia Kila Siku 8 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku hasa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Kumbukumbu la Torati, na Yohana pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz