Soma Biblia Kila Siku 8Mfano
Ni siku ya tatu tangu Yesu alipowekwa kaburini. Alikufa Ijumaa. Jumamosi ikawa sabato ya Pasaka (19:31:Wayahudi, kwa sababu ni Maandalio, miili isikae juu ya misalaba siku ya sabato, (maana sabato ile ilikuwa siku kubwa), walimwomba Pilato miguu yao ivunjwe, wakaondolewe). Na sasa ni Jumapili, siku ya kwanza ya juma(m.1). Mariamu alipoona kwamba jiwe limeondolewa akaenda haraka kutoa habari kwa Simoni Petro na kwa yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda(m.2). Yohana hataji jina lake mwenyewe, maana yeye ndiye mwandishi wa Injili hii. Hatujui walikomweka(m.2). Hasemi "sijui" bali "hatujui",maana alikuwa pamoja na wanawake wengine (Mk 16:1-2: Sabato ilipokwisha kupita, Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yakobo, na Salome walinunua manukato wapate kwenda kumpaka. Hata alfajiri mapema, siku ya kwanza ya juma, wakaenda kaburini).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 8 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku hasa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Kumbukumbu la Torati, na Yohana pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz