Soma Biblia Kila Siku 8Mfano
Baada ya kusoma mistari 18 ya kwanza ya sura hii, mambo mawili yapo wazi: 1.Kaburi ni tupu! Mwili wa Yesu haumo! (m.5-6: Yule mwanafunzi mwingine akainama na kuchungulia, akaona vitambaa vya sanda vimelala; lakini hakuingia. Basi akaja na Simoni Petro, akaingia ndani ya kaburi; akavitazama vitambaa vilivyolala.Na m.12-15: Mariamu Magdalene alisema, Wamemwondoa Bwana wangu, wala mimi sijui walikomweka. ... Naye, huku akidhania ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana, ikiwa umemchukua wewe, uniambie ulipomweka, nami nitamwondoa.)2.Sababu ya kaburi kuwa tupu ni kwamba Yesu yu hai, amefufuka! (m.16-18:Yesu akamwambia, Mariamu. Yeye akageuka, akamwambia kwa Kiebrania, Raboni! (Yaani, Mwalimu wangu). Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu. Mariamu Magdalene akaenda, akawapasha wanafunzi habari ya kwamba, Nimemwona Bwana, na ya kwamba amemwambia hayo.) Kwa kumfufua Yesu, Mungu amethibitisha kuwa yeye ndiye Mwana wa Mungu! Mungu ameipokea kazi yake ya upatanisho! Kwa njia hii Yesu alipata uwezo mkuu: wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu(Yn 1:12). Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu(m.17)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 8 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku hasa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Kumbukumbu la Torati, na Yohana pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz