Uamuzi Mkubwa Zaidi wa Maisha Yako!Mfano
“Kwa Kuhitimisha”
Kama hujawahi kumpokea Yesu katika maisha yako, au uliwahi kufanya hivyo wakati fulani,lakini huendelei kuishi kwa ajili Yake, unaweza kufanya uamuzi mpya Kwake LEO, kwa kukiri sala rahisi kutoka moyo ulio mkweli. Sala hiyo inaweza kuwa namna hii,
“Yesu, Najua ya kwamba mimi ni mwenye dhambi, na ni wewe pekee unayeweza kuniokoa na adhabu ya dhambi. Nakuomba uje katika maisha yangu na kuniosha mbali na dhambi zote. Nisaidie kuweza kuishi kwa ajili yako katika maeneo yote ya maisha yangu, kila siku ya maisha yangu. Ahsante kwa kuja katika maisha yangu na kuniweka huru!”
Kama umeomba sala hii kwa moyo wa kweli, ukiamini Yesu atafanya Aliyosema atafanya, utakuwa umepokea wokovu, na kubadili hatima yako ya milele na hivyo kuwa Naye milele! Hongera!
Kama umefanya uamuzi wa kumfuata Kristo, tungependa kusikia kutoka kwako, na kukupa masomo ya Biblia ya Kila Siku ya ziada kutoka Programu ya Biblia ya “YouVersion” na kukusaidia katika safari yako mpya. Tafadhali chagua kiunganishi cha hapo chini:
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Maamuzi mengi katika maisha huwa na athari fulani. Hata hivyo, ni uamuzi mmoja tu ndio muhimu zaidi. Kama unatafuta maelekezo rahisi ya kukuwezesha kuelewa kwa undani juu ya uamuzi huu wa ajabu – zawadi ya bure ya wokovu ya Mungu - basi anzia hapa. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo katika Kukua na Kusudi ” kilichoandikwa na David J. Swandt
More
Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2