Uamuzi Mkubwa Zaidi wa Maisha Yako!Mfano
“Sote Tunahitaji Mwokozi”
Mungu alipomuumba Adamu na Hawa, aliwaumba pasipo dhambi na katika mahusiano kamili na Yeye. Walipokosa utii kwa Mungu katika sura ya tatu ya kitabu cha Mwanzo, waliingiza dhambi katika maisha yao, na pia kwa wanadamu wote. Warumi 3:23 inaeleza juu ya athari kubwa ya uamuzi wa Adamu na Hawa.
“... kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” Warumi 3:23
Hakuna mtu asiyehusika na dhambi na athari yake, kila mmoja wetu yu katika hukumu. Matokeo yake, sisi sote tumetengwa mbali na Mungu. Dhambi zetu pia zina athari ya milele.
“Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti.” Warumi 6:23a
Kwa sababu ya uamuzi wa Adamu na Hawa wa kutomtii Mungu, kifo kikawa hakiepukiki kwao na kwa uzao wao wote (wanadamu wote); kimwili na kiroho. Baada ya kushindwa kwao, Mungu alikuwa akikabiliwa na kufanya uamuzi: kuruhusu dhambi kufanya kazi yake kwa wanadamu, kukiwa na matokeo ya kuondoa kizazi cha mwanadamu, au kutoa njia ya kumuokoa mwanadamu kutoka athari za dhambi. Ashukuriwe Mungu, ukiwa ni mwonekano wa juu wa upendo wake na neema yake, Mungu alitoa njia ya wokovu kupitia mwana wake.
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Yohana 3:16
“...bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.” Warumi 6:23b
Nje ya Yesu Kristo, hatima ya mwanadamu ni kifo cha kimwili na kiroho pia; hakuna utofauti. Lakini kwa sisi tulio ndani ya Kristo, kifo cha kimwili kinatusubiri, lakini kifo cha kiroho (jehanamu) hakitatupata. Isipokuwa, uzima wa milele Mbinguni unatusubiri baada ya kuondoka hapa duniani. Kupitia dhabihu kamilifu ya Yesu na kufufuka kwake kutoka kwa wafu, tumeepuka adhabu ya kiroho ya dhambi!
Kuhusu Mpango huu
Maamuzi mengi katika maisha huwa na athari fulani. Hata hivyo, ni uamuzi mmoja tu ndio muhimu zaidi. Kama unatafuta maelekezo rahisi ya kukuwezesha kuelewa kwa undani juu ya uamuzi huu wa ajabu – zawadi ya bure ya wokovu ya Mungu - basi anzia hapa. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo katika Kukua na Kusudi ” kilichoandikwa na David J. Swandt
More
Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2