Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Uamuzi Mkubwa Zaidi wa Maisha Yako!Mfano

Uamuzi Mkubwa Zaidi wa Maisha Yako!

SIKU 2 YA 6

“Mungu   Amekuumba Wewe Akikuwazia Umilele”
 

  Mungu alipotuumba sisi, Alikuwa na mpango wa sisi kuwa na maisha ya zaidi ya   miaka 70 au 80. Ana kusudi maalum la maisha kwa kila mmoja wetu. Mpango wake   unahusisha vyote maisha yetu ya duniani, na maisha yetu ya mbinguni (au milele).   Yakobo 4:14 inaelezea utofauti wa aina hizi mbili za maisha. Inasema,
 

  “Uzima (duniani) wenu ni nini? Maana   ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka.” Yakobo 4:14
 

  Umeshasikia ule msemo usemao, “Maisha ni mafupi.” Kulingana na umilele,   ni hivyo! Biblia inasema,
 

  “...Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu.”   Wabrania 9:27
 

  Sisi sote tunakabiliwa na kifo cha mwili. Lakini kifo cha mwili ni kusitishwa   tu kwa mwili wetu wa nyama, si nafsi zetu. Nafsi zetu, au hali ya kujitambua ya kuishi ndani yetu   ni ya milele. Nafsi zetu zitaishi milele katika moja ya sehemu baada ya kifo   cha mwili: Mbinguni au Jehanamu.
 

  Mbinguni ni paradiso ya milele, mahali ambapo Mungu anaishi.
  Jehanamu ni kutengwa kabisa mbali na Mumgu.
 

  Kuzaliwa kwetu kimwili hapa duniani haikuwa tu ndio mwanzo wa maisha yetu ya   muda hapa lakini pia maisha yetu ya kiroho hapa na baada ya hapa katika   milele yote. Kwa hiyo kuhusiana na umilele, baadhi wanaweza kuona maisha   yetu ya duniani kama yasiyo maana, lakini hilo si kweli. Hatima yako ya   milele inategemea maamuzi unayoyafanya wakati uwapo hapa duniani, muhimu   zaidi, uamuzi wa kumfanya Yesu Kristo Bwana wa maisha yako. Wokovu   unapatikana kwa sisi wote kupitia Yesu Kristo, na kupitia Yeye pekee sisi   tunaweza kubadili hatima yetu kutoka kutumia umilele wetu tukiwa tuliotengwa   na Mungu, na kuwa na umilele wa pamoja na Mungu, mbinguni. Yesu alisema:
 

  “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya   mimi.” Yohana 14:6
 

  Uamuzi tunaofanya katika maisha yetu ya duniani ni muhimu kwa sababu   zinginezo, pia. Jinsi tunavyoishi kama waamini inaweza kuwa na athari juu ya   hatima ya milele kwa wengine ambao bado hawajamjua Yesu Kristo kama Mwokozi   wao. Kila siku, wale wanaotuzunguka wanatuangalia tunavyoishi kwa ajili ya   Kristo. Kama Wakristo, Mungu anamtumia kila mmoja wetu kuileta mbingu kwa   wanaotuzunguka ambao bado hawajamjua Yeye. Yesu alisema:
 

  “Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. Wala   watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo   yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya   watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.”   Mathayo 5:14-16

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Uamuzi Mkubwa Zaidi wa Maisha Yako!

Maamuzi mengi katika maisha huwa na athari fulani. Hata hivyo, ni uamuzi mmoja tu ndio muhimu zaidi. Kama unatafuta maelekezo rahisi ya kukuwezesha kuelewa kwa undani juu ya uamuzi huu wa ajabu – zawadi ya bure ya wokovu ya Mungu - basi anzia hapa. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo katika Kukua na Kusudi ” kilichoandikwa na David J. Swandt

More

Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2