Uamuzi Mkubwa Zaidi wa Maisha Yako!Mfano
“Wokovu : Sehemu ya Mungu na Sehemu Yako”
Wokovu wako unaleta pamoja maamuzi mawili muhimu. Uamuzi wa kwanza ni ule alioufanya Mungu zamani sana wa kumleta mwanae ulimwenguni kuwa mwokozi wetu pekee. Wa pili ni uamuzi wako wa kumpokea Mwanae kama mwokozi WAKO.
“Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu – wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.” Waefeso 2:8-9
NEEMA inafafanuliwa kuwa ni kibali usichokistahili au kukifanyia kazi. Neema ni sehemu ya Mungu katika wokovu, na anatoa kibali chake kwa wanadamu kwa kumtoa Yesu aliye zawadi kamilifu. Kupitia msalaba, Yesu alilipa gharama kamili kwa adhabu ya dhambi zetu. Na kupitia Yesu, neema ya Mungu iliyofanyika mwili, hakuna kiasi cha matendo mema yanayohitajika kutoka kwetu, au tuliyowahi kulipa. Hatuwezi kuulipia wokovu wetu; ni zawadi ya bure unaopatikana kwa wote, usiohitaji malipo kutoka kwetu.
IMANI inaelezwa kuwa ni uhakika wa kuwepo kwa kitu fulani ingawa hukioni kwa dhahiri au kuweza kukigusa. Imani inahitajika kwenye upande wa sehemu yetu katika wokovu, kama tendo la utashi wetu, tunachagua kuyaachia maisha yetu kwa Mungu kwa kumfanya Yesu Bwana wa maisha yetu. Unapopokea kwa imani neema ya Mungu kupitia Yesu Kristo, bila mashaka na bila maswali, unakuwa mwenye hatima ya umilele na Mungu mbinguni. Unaweza kuwa na uhakika 100% ya ukweli huu!
Ingawa matendo mema hayawezi kutupa haki ya wokovu, yana nafasi muhimu katika maisha yetu ya Kikristo mara baada ya kumpokea Yesu.
“Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.” Waefeso 2:10
Mungu ana kusudi maalum kwa maisha yetu, undani wa jambo hilo zaidi ni wa mtu na Mungu, Lakini Mungu ana kusudi la kawaida kwa watoto wake wote, na hilo ni kule kuweka imani yetu katika matendo kwa kufanya matendo mema. Tunapofanya hivyo, tunatimiza sehemu muhimu ya mpango wa Mungu kwa maisha yetu, na tunakuwa na nafasi ya kuangaza upendo wake kwa watu wengine. Wokovu ni yote kwa pamoja, mwanzo mpya na mwisho mpya na ni sababu iletayo kusheherekea. Wewe ni kiumbe kipya, umebadilishwa milele!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Maamuzi mengi katika maisha huwa na athari fulani. Hata hivyo, ni uamuzi mmoja tu ndio muhimu zaidi. Kama unatafuta maelekezo rahisi ya kukuwezesha kuelewa kwa undani juu ya uamuzi huu wa ajabu – zawadi ya bure ya wokovu ya Mungu - basi anzia hapa. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo katika Kukua na Kusudi ” kilichoandikwa na David J. Swandt
More
Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2