Uamuzi Mkubwa Zaidi wa Maisha Yako!Mfano
“Je Mungu Akuruhusu Wewe Kuingia Mbinguni?”
Fikiria kwa muda kwamba wakati wako hapa duniani umefika mwisho bila kutazamia. Kwa mshangao, unajikuta umesimama mbele ya Muumba wako. Katika kuchanganyikiwa na matazamio na kusisimka ukitazamia hatimaye kuyaona makao yako ya milele, unasimamishwa mara kabla ya kuingia. Mungu anakuuliza swali linalopenya moyoni, “Kwa nini nikuruhusu wewe kuingia mbinguni?”
Je utajibu namna gani?
Ashukuriwe Mungu, siku ile kuu na ya ajabu itakapofika kwa kila mmoja wetu, Mungu hatatuuliza sisi kufanya mtihani fulani ili kuingia. Hata hivyo, picha hiyo inaonyesha sura muhimu, inayoleta tafakari ikikusudia kutusaidia sisi kuelewa vizuri wokovu.
Baadhi wanaweza kujibu swali la Mungu kwa kurejea mambo mazuri ambayo walifanya. Wengine wataelezea uaminifu wao wa mahudhurio kanisani, na wengine wataweka orodha ya mambo mabaya waliyoyaepuka. Pamoja na kwamba haya ni mambo muhimu ya maisha ya kila mkristo, hayatuhakikishii wokovu. Kuna jibu moja tu sahihi kwa swali hili:
“Nimemfanya Yesu Kristo kuwa Bwana wa maisha yangu, na Amenitakasa dhambi zangu zote.”
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Maamuzi mengi katika maisha huwa na athari fulani. Hata hivyo, ni uamuzi mmoja tu ndio muhimu zaidi. Kama unatafuta maelekezo rahisi ya kukuwezesha kuelewa kwa undani juu ya uamuzi huu wa ajabu – zawadi ya bure ya wokovu ya Mungu - basi anzia hapa. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo katika Kukua na Kusudi ” kilichoandikwa na David J. Swandt
More
Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2