Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Uamuzi Mkubwa Zaidi wa Maisha Yako!Mfano

Uamuzi Mkubwa Zaidi wa Maisha Yako!

SIKU 5 YA 6

“Ubatizo   wa Maji: Tamko kwa Umma la Maisha   Yaliyobadilishwa”
 

  Ubatizo wa maji ni njia muhimu ya kuutangazia umma juu ya wokovu wako.   Ubatizo wa Maji unasheherekea mwisho wa jinsi ya zamani ya maisha na mwanzo   wa aina mpya ya maisha. Yesu alifundisha umuhimu wa ubatizo wa maji kwa   wanafunzi wake kabla tu ya kupaa kwake kwenda mbinguni baada ya kufufuka.   Alisema,
 

  “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina   la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.” Mathayo 28:19

 

Agano   Jipya lote, lina simulizi nyingi za waamini kubatizwa. Ubatizo wa maji   unaonyesha ishara muhimu kwa anayebatizwa, na wao wanaoangalia. Ubatizo wa   maji unaonyesha wazi kwa watu: mwisho wa maisha yako ya zamani kwa kuzamishwa   kwenye maji, na mwanzo wa maisha mapya katika Kristo kwa kutoka ndani ya maji   uliyesafishwa, uliyetakaswa na kiumbe kipya katika Mungu.

 

Luka 3:3   inawakilisha ubatizo wa maji kama “ubatizo wa toba,” na kusisitiza umuhimu wa   kutangaza mbele ya watu kwamba tumebadilika kutoka maisha yetu ya zamani na   dhambi. Ingawa ubatizo wa maji hautuokoi wala kufunika dhambi zetu,   unawakilisha sehemu muhimu ya maisha yetu ya Ukristo – tangazo kwamba wewe ni   kiumbe kipya, maisha yaliyo badilishwa! Kama kuna mtu ambaye hakupaswa kutoa   tamko hili, basi angekuwa ni Yesu, ambaye hakuishi maisha ya dhambi hapa   duniani. Luka 3:21 inasema,
 

  “Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, Yesu naye amebatizwa,” Luka 3:21
 

  Yesu alibatizwa ili tuweze kufuata mfano wake. Ubatizo wa maji ni muhimu.   Kama hujabatizwa katika maji, unapaswa kufikiria kufanya jambo hilo kuwa ni   kipaumbele. Biblia inatuagiza sisi   kutoa tamko la wazi la wokovu wetu, na mengi ya makanisa yanayoamini juu ya   Biblia yanatoa fursa nyingi juu ya kupata ubatizo wa maji. Kufuata mfano wa   Yesu siku zote ni kujiweka katika ushindi. Mungu atakubariki sana na kukumbuka   kwa uamnifu wako na utii Kwake!

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Uamuzi Mkubwa Zaidi wa Maisha Yako!

Maamuzi mengi katika maisha huwa na athari fulani. Hata hivyo, ni uamuzi mmoja tu ndio muhimu zaidi. Kama unatafuta maelekezo rahisi ya kukuwezesha kuelewa kwa undani juu ya uamuzi huu wa ajabu – zawadi ya bure ya wokovu ya Mungu - basi anzia hapa. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo katika Kukua na Kusudi ” kilichoandikwa na David J. Swandt

More

Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2