Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutafuta KarotiMfano

Chasing Carrots

SIKU 7 YA 7

Kumtafuta Mungu

Unakwenda wapi?

Haijalishi tunakwenda wapi wakati wowote, inatusaidia kuwa na hatima akilini mwetu. 

Tatizo lilopo katika ulimwengu unaotuzunguka, ni kwamba tunasongwa na mambo ambayo tunatakiwa kuyafanya. Tunatakiwa kutafuta umaarufu na kibali na kila kitu. Kukiwa na hatima nyingi zikija kwetu, haishangazi wangapi wetu wanabaki kushangaa, wakitafuta muelekeo katika maisha.  

Kama tunaweza kuelekea kwenye hatima moja kwa wakati, hatima hiyo itakuwa wapi?

Waebrania 12:1-3 inaweka wazi. Tunatakiwa kuweka macho yetu kwa Yesu. Tunapomkimbilia, hatumpati yeye tu, lakini kila kitu tunachohitaji. Alilipa gharama kwa ajili ya dhambi zetu. Alitupatia uzima wa milele. Anatuhudumia kila siku. Na anatubadilisha kuwa watu aliotuumba tuwe.

Lakini unamkimbiliaje Kristo? Unafanya alichofanya. 

Maombi. Yesu alipotaka kupata nguvu mpya baada ya kuzungumza na watu siku nzima, alimtafuta Baba yake. Alipokuwa amesongwa katika bustani ya Getsemane, alimlilia Baba yake. maombi hutufanya kuunganika na Kristo.

Watu. Tuliumbwa kuishi kwa kushirikiana na watu wengine. Yesu alikuwa amezungukwa na watu muda wote alipokuwa hapa, akiwapa changamoto na kuwatia moyo katika imani yao. Yawezekana utafukuzia chochote ambacho watu wanaokuzunguka wanafukuzia. Kwa hiyo, kaa na watu wanaomfukuzia Mungu.

Tumikia. Jyesu alikuja duniani kutumika--ndiyo alivyosema mwenyewe. Alifanya hivyo kwa vikubwa na vidogo, na alimaliza huduma yake na kuhudumia--kuyatoa maisha yake kwa ajili yetu. Tunapowatumikia wanaotuzunguka, tunamfukuzia Mungu kwa kufanya kile Yesu alifanya.

Kufunga. Iwe Yesu alifunga kula chakula jangwani, au kwa nyakati alitoka mbele za watu na kwenda sehemu tulivu na faragha, Yesu, mwana wa Mungu, alijua wakati alipohitaji kuondoa kwa muda vitu fulani katika maisha yake kumtafuta Mungu. Wewe unaweza kuondoa kitu gani kwa muda kumtafuta mungu?

Neno. Yesu alikuwa na mwanzo hapa—kama Yohana 1 inavyosema, Kristo alikuwa ni neno la Mungu lenyewe katika mwili. Njia moja bora ya kumjua Kristo ni kukaa na yeye na mara kwa mara kusoma, kutafakari, na kufikiria uongozi wa Mungu kwetu katika Biblia.

Tenda: Ni lipi kati ya hayo juu utachukua hatua katika maisha yako? Utaanzaje? na utamwambia?

Zaidi kuhusu kumtafuta Mungu. 

siku 6

Kuhusu Mpango huu

Chasing Carrots

Wote tunatafuta kitu. Mara nyingi ni kitu ambacho hakipatikani--kazi nzuri, nyumba bora zaidi, familia bora, kukubalika na wengine. Lakini hii haichoshi? Je, kuna njia bora zaidi? Pata katika mpango wa new Life.Church Bible, ikifuatana na mfululizo wa ujumbe wa Mchungaji Craig Groeschel’s, Kutafuta Karoti.

More

Tunapenda kuwashukuru Life.Church kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tuvuti ya https://www.life.church/