Kutafuta KarotiMfano
Kutafuta Mafanikio
Inapokuja kuhusu wafalme wa kibiblia, hakuna aliyafanikiwa kama Sulemani. Israeli ilistawi chini ya utawala wake. Alisimamia ujenzi wa hekalu la Mungu. Alijijengea mwenye ikulu ya kifalme. Watawala walisafiri umbali mrefu kuja kuangalia utajiri wake, wakileta zawadi za dhahabu na vito. Aliweza kujibu kila swali aliloulizwa. Alichagua aina ya wanawake. Alibarikiwa na kila kitu chema ambacho kila mtu angetamani kuwa nacho katika maisha yake.
Kama kuna mtu angekuwa na furaha kwa kile alichofanikiwa katika maisha, angekuwa Sulemani. Lakini katika kitabu cha Mhubiri, Sulemani alionesha picha tofauti. Alisema , " Nami nikaichukia kazi yangu yote niliyojishughulisha nayo chini ya jua..." anaeleza, "kwa sababu lazima niviache kwa mtu ajae baada yangu."
Sulemani alifikiria jambo. Hatuwezi kubeba vyote katika maisha yajayo. Kupandishwa vyeo, nyumba, tuzo, magari, na likizo vyote hubaki.
Unafikiria sasa nini ni muhimu katika maisha?
Sulemani alipata jibu kwa swali hilo. Mwiso wa Mhubiri,, anamalizia, "Mche Bwana , nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.”
Kwa mtazamo wa haraka, hii inaweza isionekane si kitu cha msukumo, lakini chukua kitabu kingine. Sulemani anasema kwamba hivi ndivyo vitu tunavyotakiwa kuvitafuta kufanikiwa maishani: kumcha Mungu--ikimaanisha kumpenda, kumtii, na kufanya anachokutaka ufanye.
Tumezoea msemo wa ulimwengu, “Kimbia, usisimame. Unaona vitu hivi vya thamani? Angalia sifa zote hizi? Maelfu ya watu wanataka, lakini wasikusimamishe. Vipiganie! Nenda! Unafanya nini kingine na maisha yako? Maisha ni mashindano, na walio bora watashinda.”
Lakini neno la Mungu linasema, “Mpende Mungu. Fanya vyema.”
Fikiria ni jinsi gani hii inapatikana kwa kila mtu. Haijalishi wewe umeoa/umeolewa ama la. Tajiri au Maskini. Kijana ama mzee. Mzima au mgonjwa. Mpende Mungu na fanya vyema.
Fikiria: Kitu gani utabadirisha leo kama lengo lako kuu katika kila hali ni kumpenda Mungu na kufanya vyema? Utafikiaje lengo hili?
Kuhusu Mpango huu
Wote tunatafuta kitu. Mara nyingi ni kitu ambacho hakipatikani--kazi nzuri, nyumba bora zaidi, familia bora, kukubalika na wengine. Lakini hii haichoshi? Je, kuna njia bora zaidi? Pata katika mpango wa new Life.Church Bible, ikifuatana na mfululizo wa ujumbe wa Mchungaji Craig Groeschel’s, Kutafuta Karoti.
More