Kutafuta KarotiMfano
Kutafuta Karoti
Wazo la kutafuta Karoti linatoka kwenye mfano wa karoti na kijiti ambao uliandikwa kwa mara ya kwanza katikati ya mwaka-1800. Hebu fikiria katuni akishuka kwenye punda na kuning'iniza karoti ambayo haiwezi kufikiwa. Mwendesha Punda anashikilia karoti katika kijiti kirefu na anakitumia kumshawishi punda kukimbia. Kwa punda, zawadi yake ni hatua moja mbele.
Unajisikia kama punda?
Kabla ya miaka hiyo 1800, Mfalme Suleiman alilalamika kuwa kutafuta bila mafanikio katika maisha ni zaidi ya "kufukuza upepo."
Umewahi kujaribu kutaka kuukamata upepo? Ni kupiga hatua moja mbele zaidi.
Kitu cha kuangalia zaidi kuhusu " Hatua moja zaidi" ni kwamba sikuzote ni hatua moja zaidi. Miaka mingi kidogo katika kazi hii, au mara unapohitimu, au mara unapooa au kuolewa, au watoto wanapokua, au wakati imani yako inaimarika, au unapoweza kitu kinachokupa furaha. Ni. Hatua. Moja. Zaidi.
Kuna njia bora zaidi ya kuishi. Unaweza kushuka katika duara la utendaji. Kuna vitu vingi katika maisha zaidi ya kikubwa na bora.
Yesu alilisemea zaidi hili la kutafuta katika Mathayo 6. Unaposoma maneno ya Yesu leo, jaribu hili. Vuta pumzi kwa nguvu ndani na ondoa kinachokusumbua akili mwako. Fikiria upo mahali ambapo Yesu anafundisha. Umekalia kitu gani? Kuna harufu gani hapo? Na sauti yake inasikikaje? Unasikia nini tena? Unaona nini? Kitu gani kinafumuka ndani yako unaposikia sauti yake?
Baada ya kumaliza kusoma maandiko ya leo kwa njia hiyo juu, hapa kuna maswali mawili ya kutafakari. Ilikuwa vyema kupunguza mwendo na kuwa karibu na Yesu? Nawezaje kutoa nafasi zaidi maishani kwangu kwa Yesu?
Omba: Baada ya kusoma maandiko ya leo, omba na kumuomba Mungu apunguze mwendo wako ili uweze kumsikia siku nzima.
Angalia video, miongozo ya majadiliano, na zaidi kuhusu Kufukuzia Karoti.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Wote tunatafuta kitu. Mara nyingi ni kitu ambacho hakipatikani--kazi nzuri, nyumba bora zaidi, familia bora, kukubalika na wengine. Lakini hii haichoshi? Je, kuna njia bora zaidi? Pata katika mpango wa new Life.Church Bible, ikifuatana na mfululizo wa ujumbe wa Mchungaji Craig Groeschel’s, Kutafuta Karoti.
More