Kutafuta KarotiMfano
Kutafuta Ukamilifu
“Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu" Mathayo 5:48
Si jambo kubwa, sawa? Unatakiwa kuwa mkamilifu--kama mtakatifu, mkamilifu Mungu wa mbingu na nchi aliyo mkamilifu.
Si jambo kubwa, sawa?
Ndiyo, si kitu.
Kama utajifanya mkamilifu, utaanzia wapi? Mungu ni mkamilifu kwa sababu hana dhambi, au makosa, ndani yake. Tunazungumza juu ya mawazo ya dunia kuhusu ukamilifu hapa-- mavazi mazuri, nyumba nzuri, mwenza mzuri. Tunachozungumza hapa ni juu zaidi ya hivyo. Utatakiwa kuwa hunadhambi. Hakuna kudanganya, kulaani, kuwabugudhi watoto, au "kuazima" nywila ya Netflix ya rafiki yako.
Hebu jifanye unasema, “Hakika. Naweza kufanya hivyo.” Na unafanya. Unafuta kitendo chako. Unatii kiwango cha mwendo. Unawapa masikini. Unalipia Netflix mwenyewe. Na unafanya hivyo kwa siku, kwa juma, kwa miezi, mwishowe miaka.
Lakini bado usingekuwa mkamilifu.
Angali, kuna mambo madogo ya dhambi ambazo umetenda. Kama Yakobo 2:10 inavyosema --Maaana mtu awaye yote atakayeshika sheria yoye, ila akajikwaa kwa neno moja, amekosa juu ya yote.
Sasa, unaenda wapi kutoka hapa?
Katika Mathayo 19, kijana tajiri alijikuta akitaka kuwa mjanja. Alimuuliza Yesu nifanye nini ili niupate uzima wa milele. Yesu alimwambia azishike amri kuu. Yule kijana akasema nimezishika zote toka utoto wangu. Ndipo, Yesu akamjibu, "ukitaka kuwa mkamilifu, nenda, ukauze ulivyo navyo uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo unifuate." Lakini yule kijana aliposikia neno lile, akaenda zake kwa huzuni, kwa sababu alikuwa na mali nyingi.
Yesu hakuwa anamwambia kijana kwamba kuwa mkamilifu ni hatua mbili. Kwanza, tii amri, na pili, toa ulichonacho. Yesu alikuwa anasema njia ya kwendea ukamilifu inaanza na kuachana na chochote kinachoweza kukuzuia kumfuata yeye.
Lakini ukamilifu? Yawezekanaje mtu kuwa mkamilifu? Huu si aina ya ukamilifu wa duniani. Ni bora zaidi. Unapochagua kumfuata Kristo, huzifunika dhambi zako na kutokukamilika kupitia mauti aliyokufa msalabani. Na machoni pa Mungu, unakuwa mkamilifu ndani yako kama Kristo mwenyewe.
Omba: Mungu, asante kwa dhabihu kamili ya mwana wako. Nisaidie kuacha chochote kinachonizuia kumfuata Kristo. Katika jina la Yesu, Amen.
Kuhusu Mpango huu
Wote tunatafuta kitu. Mara nyingi ni kitu ambacho hakipatikani--kazi nzuri, nyumba bora zaidi, familia bora, kukubalika na wengine. Lakini hii haichoshi? Je, kuna njia bora zaidi? Pata katika mpango wa new Life.Church Bible, ikifuatana na mfululizo wa ujumbe wa Mchungaji Craig Groeschel’s, Kutafuta Karoti.
More