Kutafuta KarotiMfano
![Chasing Carrots](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F14957%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Kutafuta Faraja>
Ikiwa tumesongwa, kuumizwa, tumechoka, wapweke, au tupotupo tuu, wote tunajikuta wakati fulani tunatafuta faraja. Nani ambaye hajatumia fedha zaidi, hajavimbiwa, amelala sana, amekunywa kupitiliza, na kukadiria zaidi uwezo wa kitu ili kuleta faraja ya kudumu?
Neno “faraja” lina historia ngumu. Linatokana na sehemu za maneno mawili ya Kilatini, com-, likimaanisha “pamoja na,” na fortis, likimaanisha “enye nguvu au nguvu.” Baadaye, neno la Kilatini confortare lilikuja kumaanisha “kutia nguvu zaidi.” Mwishowe, neno la zamani la Kifaransa, conforter, liliongeza maneno kama “faraja” na “msaada” kwenye ainisho. Katika karne ya 14, neno lingine la Kifaransa conforten liliainishwa kama “changamka, faraja.” Mwishowe, kwenye karne ya 17, toleo la Kiingereza ya neno ilianza kumaanisha hali ya kustarehe kimwili ambayo tunaielewa leo.
Kwa nini hili ni muhimu? Kama baada ya miaka mia moja, neno “faraja” lilitoka kwenye maana ya “pamoja-kutia nguvu,” kwenda kumaanisha “mkinga- maumivu.”
Je, unamuona Mungu kama nguvu yako, pamoja na wewe katikati ya maumivu, au kama mkinga maumivu?
Nabii Isaya alitabiri juu ya Masihi atakayeingia ulimwenguni ili kuchubuliwa kwa ajili ya makosa yetu na kuteseka ili tupone. Kama asili ya imani yetu ni kufuata hatua za Yesu, basi tufikirie anavyoyapokea maumivu. Katika Petro 2:21-25, tunamwona Mwokozi aliyepokea maumivu kimya kimya pamoja na kwamba hakufanya kitu kuyastahili. Yesu hakwepi maumivu, au kutafuta mbadala; anakuja ulimwenguni kwetu na kufanya maumivu yetu ya kwake.
Yesu ni nguvu-pamoja. Ndipo, kabla hajaenda kuwa pamoja na Baba, anatuahidi kwamba Roho Mtakatifu --"Mfariji" --hatakuwa pamoja nasi tuu, lakini ndani yetu! Hicho ni kitu kinachostahili kufukuziwa.
Kwa hiyo, tusitafute aina ya faraja ya dunia—kufuata Netflix series na rafiki zetu Ben & Jerry. Badala yake, tutafute faraja kutoka kwa Roho Mtakatifu, tukijua kwamba haimaanishi maisha ya kutokuwa na maumivu lakini faraja katikati ya maumivu.
Omba: Mungu, sipendi maumivu, lakini nakupenda. Tafadhali badilisha ufahamu wangu wa faraja yako, na unisaidie kwa uhuru kuihisi. Roho Mtakatifu, nioneshe jinsi "nguvu- pamoja" iko nami na ndani yangu. Yesu, asante kwa kubeba aibu yangu msalabani. Amen
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![Chasing Carrots](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F14957%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Wote tunatafuta kitu. Mara nyingi ni kitu ambacho hakipatikani--kazi nzuri, nyumba bora zaidi, familia bora, kukubalika na wengine. Lakini hii haichoshi? Je, kuna njia bora zaidi? Pata katika mpango wa new Life.Church Bible, ikifuatana na mfululizo wa ujumbe wa Mchungaji Craig Groeschel’s, Kutafuta Karoti.
More