Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutafuta KarotiMfano

Chasing Carrots

SIKU 2 YA 7

Kutafuta Umaarufu

Neno la kiyunani la umaarufu—phēmē, likitamkwa fā'-mā—limetumika mara mbili tuu katika Agano Jipya. Mara nyingi limeainishwa kama hotuba, taarifa, au habari. Hivi ndivyo phēmē unatumika katika Luka 4:14:

Na Yesu alirudi Galilaya katika nguvu ya Roho Mtakatifu: na ukatoka umaarufu wake katika miji yote iliyozunguka.

Yesu alikuwa anarejea kutoka wapi kulikosababisha umaarufu wake kuenea katika eneo lote? Katika Luka 1, tunasikia habari za kuzaliwa kwa Yesu. Katika Luka 2, anazaliwa na kuwa kijana. Katika Luka 3, anabatizwa. Mwishowe, katika mistari kadha ya mwanzo ya Luka 4, Yesu anafunga na kujaribiwa nyikani na shetani. Hii inaturudisha kwenye Luka 4:14.  

Ndipo Yesu akarudi Galilaya, akiwa amejawa na nguvu ya Roho Mtakatifu. Taarifa kumhusu zilisambaa haraka katika eneo lote. Luka 4:14  

Katika maandiko ya leo, utaichukua habari nzima ya majaribu ya Yesu nyikani. Yesu alikuwa anafunga jangwani kwa siku 40 na katikati ya hilo, shetani mwenyewe alimjaribu na chakula kisichofaa (Luka 4:3-4), umaarufu (Luka 4:5-8), na imani (Luka 4:9-12). Kila mara, Yesu alikataa jaribu na alijibu kwa neno la Mungu.

Luka 4:14 umaarufu siyo siku zote ndiyo tunaotafuta, si ndiyo? Tunaelekea kufuata kufuata majaribu shetani alimjaribu Yesu nyikani. Chakula bila utoshelevu (Luka 4:3-4), milki bila sadaka (Luka 4:5-8), na wokovu bila kujisalimisha (Luka 4:9-12). 

Fikiria kutambuliwa kazini, kukubalika kwenye mitandao ya kijamii, na sifa kutoka kwa watu. Unajisikia vizuri kwa Muda, na mara unatamani tena zaidi. Kama tukiwa wa kweli, wote tumepitia nyakati ambapo tumetaka kutambuliwa au kujulikana kwa ajili ya jambo fulani. vivyo hivyo, shetani alimwahidi Yesu fedha, umaarufu, na mamlaka. Yesu alijaribiwa kama sisi, lakini hakutii majaribu. 

Pia tutasoma kuhusu jaribu la mwisho la shetani kwa Yesu--akimtaka kuruka kutoka kwenye kinara cha jengo ili Mungu amuokoe. Je, umewahi kuomba ombi ambalo linamlazimisha Mungu kufanya vitu kama unavyotaka, kwa muda unaotaka. Si jambo la heshima kwa Mungu--ndiyo maana Yesu alijibu kwa kusema tusimjaribu Mungu namna hivyo.

Kuna lugha iliyoundwa upya inaitwa PIE—Proto-Indo-European—Babu asiyeandikwa wa Uyunani. Neno la msingi la PIE ambali lilikuja kuwaphēmē, is -bha, likimaanisha “kuangaza” na “kusema.” Hebu turudi kwenye asili zetu. Hatujaumbwa kuwa nuru—huyo ni Yesu--lakini tumeitwa kuangaza nuru yake. Sisi siyo neno--injili ya Yohana inasema hilo pia ni Yesu—lakini tumeitwa kusema neno lake kwa ulimwengu mzima.

Kutafuta umaarufu ni kutafuta kitu ambacho ni mali ya Mungu badala ya kumtafuta Mungu mwenyewe. Hilo ni jaribu la zamani zaidi katika kitabu. Usianguke katika hilo. Utakapopata jaribu la umaarufu, fanya kama Yesu alivyofanya. Angaza nuru ya Mungu kwa kusema maneno yake. Na utakapofanya, Luka 4:14 inatokea. Umaarufu wake unatawanyika kuzunguka.

Omba: Mungu, jinsi unavyopenda kunifanya niangaze nuru yako? Nataka nikufuate kwa kila kitu ndani yangu. Amen.  

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Chasing Carrots

Wote tunatafuta kitu. Mara nyingi ni kitu ambacho hakipatikani--kazi nzuri, nyumba bora zaidi, familia bora, kukubalika na wengine. Lakini hii haichoshi? Je, kuna njia bora zaidi? Pata katika mpango wa new Life.Church Bible, ikifuatana na mfululizo wa ujumbe wa Mchungaji Craig Groeschel’s, Kutafuta Karoti.

More

Tunapenda kuwashukuru Life.Church kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tuvuti ya https://www.life.church/