Soma Biblia Kila Siku 4Mfano
Si ajabu kwamba Waisraeli waliogopa walipoliona lile jeshi kubwa la Farao. Walifanya vema walipomlilia Bwana (m.10b). Ila baada ya kumlilia Bwana hawakumngojea, bali walimshtaki Musa kwamba amewaelekeza jangwani, mahali pa kufa tu (m.11-12). Katika hili sisi tujifunze kwamba tukimlilia Bwana, pia tulingojee jibu lake. Tusubiri na kuona jinsi atakavyotuokoa. Musa aliwahakikishia Waisraeli kuwa wataokolewa na Bwana (m.14). Kisha Musa aliambiwa ainue fimbo yake na kuigawanya bahari ili waweze kupita (m.15-18).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 4 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu, hasa kutoka Kitabu cha Kutoka, na 1 Wathesalonike, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz