Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 4Mfano

Soma Biblia Kila Siku 4

SIKU 13 YA 30

Mungu alikuwa hajamaliza kujipatia utukufu kwa njia ya Farao. Alimwambia Musa kwamba Waisraeli warudi na kupiga kambi mahali palipoonekana pabaya machoni pa Wamisri. Hivyo ilionekana kana kwamba Waisraeli wamepotea njia, yaani ni kama walikuwa wanazuiliwa na jangwa wasiweze kutoka (m.3-4). Farao na watumishi wake waliposikia habari hiyo, mioyo yao iligeuka. Mioyo yao ilifanywa migumu na Mungu ili aweze kuonyesha utukufu wake. Hivyo Farao aliwafuata Waisraeli pamoja na jeshi lake kubwa (magari mia sita siku zile yalikuwa mengi mno, ni jeshi kubwa sana).

siku 12siku 14

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 4

Soma Biblia Kila Siku 4 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu, hasa kutoka Kitabu cha Kutoka, na 1 Wathesalonike, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha