Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 4Mfano

Soma Biblia Kila Siku 4

SIKU 10 YA 30

Mungu aliwapa Waisraeli amri kuhusu mlo wa Pasaka. Katika kula pasaka wasiotahiriwa walitengwa, wasile pasaka. Kula pasaka ni kwa watu wa Mungu tu. Tohara ni mfano wa ubatizo. Katika Chakula cha Bwana twapata ondoleo la dhambi. Ni kwao waliompokea Kristo, lakini tunawaalika wote wampokee Yesu Kristo ili wapate baraka tunazopata sisi.Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo; basi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochachika, ndio weupe wa moyo na kweli(1 Kor 5:7-8). Tukumbuke kuwa hatuwezi kushiriki Chakula cha Bwana tukiwa tunaishi katika dhambi. Tumwungamie Yesu dhambi zetu tukiziweka wazi mbele yake na kuziacha!

siku 9siku 11

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 4

Soma Biblia Kila Siku 4 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu, hasa kutoka Kitabu cha Kutoka, na 1 Wathesalonike, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha