Soma Biblia Kila Siku 1Mfano
Wakati wa Yakobo, idadi ya watu wa familia yake ilikuwa 70 tu. Lakini kutokana na baraka ya Mungu, idadi ya Waisraeli waliotoka Misri ilikuwa mnamo laki siti (Kut 12:37). Muda wa kukaa katika Misri ulikuwa miaka 430 (Kut 12:40). Leo tujifunze mambo mawili: 1. Waisraeli waliishi katika nchi ya kigeni kwa muda mrefu, tena waliteswa na Wamisri. Lakini Mungu hakuwasahau Waisraeli, bali hatimaye aliwakumbuka, akawaokoa. 2. Chuki ya maadui wa Mungu haimzuii Mungu kuwabariki watu wake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 1 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu, hasa kutoka Injili ya Yohana, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz