Soma Biblia Kila Siku 1Mfano
Wayahudi walitaka kumwua. Ndugu zake hawakumwamini (m.5) wala kumpenda. Maana walimpa Yesu ushauri ambao walijua utampambanisha na Wayahudi. Swali muhimu la kujiuliza ni, “Kwa nini hao walimchukia Yesu?” Soma tena m.7! Watu wa ulimwengu huu humchukia Bwana Yesu kwa sababu anawaambia ukweli. Mimi na wewe tunapokeaje ushuhuda wake juu yetu? Tukiupokea tutachukiwa na watu wa ulimwengu huu kwa sababu wanamchukia Yesu. Lakini tuhesabu tuna heri, maana neno lake ni kweli (ling. Mt 5:11-12).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 1 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu, hasa kutoka Injili ya Yohana, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz