Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ngumu na Lisa BevereMfano

Adamant With Lisa Bevere

SIKU 2 YA 6

Hakuna mtu anayekua bila kuguswa na giza. Sote twasikia sauti zinazotuzunguka kwa kiasi fulani, zinazotuhukumu na kutubandika. Wengi wetu, kama si wote, wamejibandika pia—utambulisho wa uongo ambao tutaapa kwamba ni kweli. 

Mungu anapojongea karibu nasi, si kutuhukumu, bali ni kujikusanyia sisi kwake kwa uhusiano wa karibu sana ili tuweze kusikia sauti yake ikitamka ukweli wa utambulisho wetu. 

Ukweli ni kwamba: sisi si giza ya kale yetu. Na hatufafanuliwi na makosa yetu, jinsia, ama kitu chochote cha nje. Badala yake, sisi ni roho zilizoumbwa katika mfano wa Mungu, ili kuwa na uhusiano wa karibu sana na Yeye aliyetupa pumzi. 

Tunasahau utambulisho wetu tunapouambatanisha na vitu visivyofaa. Kwa sababu hii, Mungu ataondoa mabandiko yanayozuia ambayo tumeokota njiani. Roho yake itafanya kazi ndani yetu, ikitoa ya kale na kufunua yale ambayo bado hayajaonekana. 

Pengine woga na wasiwasi imekufanya ukatae kazi ya Mungu maishani mwako. Lakini leo, Mungu anazungumzia sehemu hizo ambazo ulidhani kwamba ni tasa, na anajitolea kuzigeuza kuwa bustani tena. 

Lakini lazima tuwe tayari kumruhusu Mungu kutenganisha nuru na giza maishani mwetu. Mungu hataruhusu uongo ambao umezungumziwa juu yako kubaki. Hataruhusu vitu ambavyo umejizungumzia juu yako mwenyewe kuwa kauli ya mwisho. Badala yake, atajongea karibu nawe ili aweze kufunua kitu kipya ndani yako katika uhusiano wa karibu sana, kitu ambacho kinaleta uponyaji kamili wa kila sehemu ya maumivu, kukuachilia huru kuishi katika ukweli ule ambao Mungu anasema ni utambulisho wako. 

Mungu ni mgumu kwa kutaka uhusiano wa karibu sana. Ataenda kwa kiini cha maumivu yako ili kukuponya, lakini lazima umruhusu aingie afanye hivyo. Je, kufanya huku kunakaa aje maishani mwako?

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Adamant With Lisa Bevere

Ukweli ni nini? Wanadamu wameanza kuamini uongo kuwa ukweli ni mto, unaopwa na kutiririka na upitaji wa wakati. Lakini ukweli si mto—ni jiwe. Na katika bahari inayochacha ya maoni, mpango huu utakusaidia kutia nanga ya moyo wako—kukupa mwelekeo katika ulimwengu unaozurura.

More

Tungependa kuwashukuru John na Lisa Bevere kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://iamadamant.com