Ngumu na Lisa BevereMfano
Tunapopokea upendo wa Mungu, jibu la kawaida zaidi na la lazima ni kwamba tutoe upendo. Tunafaa kupenda bila woga, kwa ushindi, na milele. Ithibati ya kweli ya mtu anayejua kuwa anapendwa ni kwamba anapenda vyema.
Si kwamba Mungu ana upendo; yeye ni upendo. Upendo ni hali yake yenyewe. Na kwa sababu Mungu ni upendo, huwezi kumfanya Mungu aache kukupenda. Upendo wake haishindiki wala kusongesheka, haitikisiki na kupwa na kujaa kwako.
Lakini kwa sababu Mungu anapenda kila mtu, hawezi kupenda kila kitu. Kwa sababu Mungu ni mgumu katika upendo, lazima pia awe mgumu katika chuki.
Pengine hii inaonekana kuwa kinaya mwanzoni, lakini hii ni kwa sababu jamii yetu imefanya upendo kuwa kama sanamu. Tunajua kwamba Mungu ni upendo, lakini tumeweka dhana yetu ya upendo kuwa mungu?
Ukweli ni kwamba, Mungu anachukia yale yanayoumbua upendo. Anachukia vitu ambavyo vinavyoangamaiza wale ambao anawapenda. Hii ndio sababu sharti Mungu anachukia vitu vyovyote vinavyopotosha utambulisho wetu.
Maandiko yanatuambia pia Mungu anachukia: kila kitu kinachozuia haki na ukweli, wajane na mayatima wanapodhulumiwa, unyanyasaji wa wazee na kupuuza kwa familia, yanayopotosha uzuri wake na kuchafua zawadi zake, upendo unapogeuzwa kuwa ubinafsi na marafiki wanaogeuka kuwa adui, yanayobadilisha taswira yake na kupotosha yetu, wakati ambapo ubaya unaitwa wema na watu wasio na hatia wanapouawa, na kiburi na majivuno yanapotushusha hadhi. Kwa kifupi, Mungu anachukia yote yanadhoofisha upendo, kwani chochote kinachoharibu upendo kinatuharibu pia.
Hatuwezi kuwa na upendo wa kweli ikiwa “tunapenda kila kitu.” Mungu ni mgumu katika upendo na chuki, kwa hivyo lazima tujifunze kupenda yale ambayo Mungu anapenda na kuchukia yale anayochukia.
Ni katika njia zipi jamii yetu imefanya dhana yake ya upendo kuwa mungu? Mungu anapenda kila mtu, lakini hapendi kila kitu. Unaona ukweli huu vipi maishani mwako?
Kuhusu Mpango huu
Ukweli ni nini? Wanadamu wameanza kuamini uongo kuwa ukweli ni mto, unaopwa na kutiririka na upitaji wa wakati. Lakini ukweli si mto—ni jiwe. Na katika bahari inayochacha ya maoni, mpango huu utakusaidia kutia nanga ya moyo wako—kukupa mwelekeo katika ulimwengu unaozurura.
More