Ngumu na Lisa BevereMfano
Mungu anakuambia, “Wewe ni mgumu wangu.” Haijalishi ikiwa huhisi kwamba u mgumu wakati huu; umezingirwa katika kazi ya Kristo isiyoweza kuangamizwa. Sikia baadhi ya matamko ambayo Mungu anasema juu yako leo:
Wewe ni mgumu wangu, imara ilhali wazi—watu wanaweza kutazama kupitia kwako na kuona Kristo.
Wewe ni mgumu wangu—Roho wa Kristo anaishi ndani ili uwe mtu asiyesongesheka wala kutikisika.
Wewe ni mgumu wangu—una nafsi ya moto!
Yesu alikuja kutubatiza na Roho Mtakatifu na kwa moto. Huu ni ubatizo ambao ni lazima tupokee. Tunapookoka, mioyo yetu yasiyo na uhai inahuishwa na ung'aavu wa upendo wake unaodumu milele.
Hujui jinsi unavyoonekana kiroho. Unafikiri kwamba unazungumza maneno tu, lakini unazungumza moto! Unatamka vitu ambavyo vinatenganisha kwa mwangaza na ukweli uongo wa adui ambao watu wamekuwa nao kwa muda mrefu sana. Unazungumza moto unaoyeyusha minyororo. Unahitaji kusimama katika ukweli huu.
Zawadi iliyopo maishani mwako ni kama moto. Usiuruhusu uzimike. Puliza makaa na uyapepee yawe moto mkuu! Wengine wanahitaji moto huo uwake na kuangaza ndani yako na kutoka kwako, kwa sababu wewe ni mwana wake, aliyezaliwa upya katika asili yake.
Mungu anakuongelesha kulingana na jinsi utakavyokuwa, wala si jinsi ulivyo. Anaaminia sana mpango wake wa maisha yako. Kwa kuzingatia hayo, ni vitu vipi ambavyo unahitaji kuacha (ama kuanza) kuzungumza juu yako?
Ikiwa ulifurahia mpango huu wa kusoma, ninakuhimiza uchunguze zaidi kwa kutazama kitabu changu kipya Adamant: Finding Truth in a Universe of Opinions.
Kuhusu Mpango huu
Ukweli ni nini? Wanadamu wameanza kuamini uongo kuwa ukweli ni mto, unaopwa na kutiririka na upitaji wa wakati. Lakini ukweli si mto—ni jiwe. Na katika bahari inayochacha ya maoni, mpango huu utakusaidia kutia nanga ya moyo wako—kukupa mwelekeo katika ulimwengu unaozurura.
More