Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ngumu na Lisa BevereMfano

Adamant With Lisa Bevere

SIKU 4 YA 6

Unataka kuwa na umaarufu . . . ama ushawishi? 

Umaarufu na ushawishi unaonekana kufanana, lakini ni tofauti sana. Umaarufu unahitaji ufuate umma na kuwaambia yale ambayo wanataka kusikia. Lakini ushawishi unakualika kusimama katika ukweli mbali na umati.

Katika kiini chake, ukweli si nini, bali ni nani, kwa sababu Yesu alisema kwamba yeye ni ukweli. Yesu alisema pia kwamba Neno la Mungu ni ukweli. Ulimwengu unapenda kufikiria kwamba ukweli unabadilikabadilika na ni tegemezi, lakini ukweli umekita mizizi katika mtu ambaye ni Yesu na Neno la Mungu halibadiliki kamwe. Katika ulimwengu uliojaa maoni, ukweli wa Mungu utatuongoza kupata kanuni za kujengea maisha yetu. 

Lazima tuwe makini kutambua tofauti kati ya maoni na kanuni. Ulimwengu wetu hauhitaji fujo unaotokana na maoni mengi. Unahitaji uthabiti unaotokana na ukweli. Tusichangie kelele unaokengeusha fikra na kutuzuia kutazama Maandiko na Roho wa Kweli.

Maoni ni rahisi kuunda na haraka kubadilisha, lakini ngumu kusafisha ikiwa tumekuwa tukiyaeneza maoni yetu kiholela. Yanaweza kuwa kama takataka inayochafua maisha yetu na ya wengine. Lazime tuwe makini kuchunga maneno yetu kuhakikisha kwamba tumo miongoni mwa suluhisho za matatizo ambazo tumepakwa mafuta kubadilisha.

Ninakuhimiza uhariri maisha yako na maneno unayochagua kunena. Uwe mwangalifu na yale ambayo unasoma, unasikiliza, unasoma, ama kuchapisha. Usitangaze mambo ya familia yako, ama mambo ya kanisa yako, ili ulimwengu wote usikie. Hata hivyo, usinyamaze kuyahusu: zungumza na familia kuhusu mambo ya familia. Usiwahusishe watu ambao hawana uhusiano na tatizo ama suluhisho ikiwa huwahitaji. Hii inazidisha tatizo badala ya kulitatua. 

Ni vipi kwamba kubaki kimya kuhusu masuala muhimu ni sawa na kuyaunga mkono? Kuhariri maneno yako ili uwe miongoni mwa suluhisho badala ya tatizo kuna maana gani? 

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Adamant With Lisa Bevere

Ukweli ni nini? Wanadamu wameanza kuamini uongo kuwa ukweli ni mto, unaopwa na kutiririka na upitaji wa wakati. Lakini ukweli si mto—ni jiwe. Na katika bahari inayochacha ya maoni, mpango huu utakusaidia kutia nanga ya moyo wako—kukupa mwelekeo katika ulimwengu unaozurura.

More

Tungependa kuwashukuru John na Lisa Bevere kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://iamadamant.com