Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ngumu na Lisa BevereMfano

Adamant With Lisa Bevere

SIKU 5 YA 6

Mara nyingi kanisa ni nyepesi kulaani wasio waamini kwa dhambi na tabia zao, ingawa si ajabu kwamba watu ambao hawajui Mungu wanatenda kana kwamba hawamjui Mungu. Tunachofaa kujihusisha nacho, kwanza kabisa, ni ikiwa tunaishi maisha matakatifu na yaliyobadilika. Tunaposaka Bwana, ndipo tunapoweza kuomba hekima ya kufunua ukarimu wake duniani tunamoishi kwa njia ambayo inawaalika kutafuta kubadilika wenyewe kwake. 

Kama watoto wa Mungu, tumeumbwa upya ndani ya Kristo kuwa mgumu kama almasi ila mwororo kama ua. 

Tunaishi katika ulimwengu ambao ni timizo la maandiko ya Paulo katika Warumi 1. Wengi wetu wameasi ujuzi na uwepo wa Mungu na hatuwezi kutambua tena mambo ya kimsingi ya mpango wake kwa wanadamu.

Lakini jiulize, kusikitika kuhusu maovu ya siku hizi umewahi kubadilisha kitu chochote? Cha kusikitisha ni kwamba, tumejulikana zaidi kwa yale ambayo tunapinga kuliko yale ambayo tunaunga mkono. Utakatifu na mabadiliko ambao tunatafuta katika jamii yetu hautatokana na kuihukumu wala kuilaani, bali utatendeka tunapotatua shida zetu kwanza kisha kuachilia ukarimu, huruma, na tumaini ya Mungu kwa wale ambao wanaihitaji. 

Ukarimu wa Mungu daima ni mwaliko kwetu turudi kwa ukweli, wala si idhini kwa dhambi. Wakati mwingine, tunatenda kana kwamba ni fadhila kusema kwamba dhambi si dhambi kwa sababu hatutaki watu kuona haya. Lakini, tunahitaji kuwa tayari kuita dhambi dhambi bila kupindapinda, ingawa kuifanya kwa njia ambayo inaleta tumaini badala ya hukumu. 

Utakatifu katika jamii yetu unaanza na sisi kujitolea kikamilifu kwa Mungu. Kuna kizazi ambacho kinahitaji mabadiliko, na wanangoja kuyaona ndani yetu. 

Mungu anasema kwamba ataponya nchi watu wake wanaponyenyekea na kuomba, wala si wakati ambapo kila kitu katika serikali ya nchi hiyo ni kamilifu. Hii ina maana gani kwako? 

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Adamant With Lisa Bevere

Ukweli ni nini? Wanadamu wameanza kuamini uongo kuwa ukweli ni mto, unaopwa na kutiririka na upitaji wa wakati. Lakini ukweli si mto—ni jiwe. Na katika bahari inayochacha ya maoni, mpango huu utakusaidia kutia nanga ya moyo wako—kukupa mwelekeo katika ulimwengu unaozurura.

More

Tungependa kuwashukuru John na Lisa Bevere kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://iamadamant.com