Oswald Chambers: Furaha- Nguvu katika BwanaMfano
Hakuna kitu kinachoudhi kama ushauri, “tabasamu”; ni bandia, mwanga unaofifia haraka. Kitu kimoja ambacho Yesu Kristu anamfanyia mtu ni kumfanya ang'ae, na si bandia. Furaha ambayo Yesu anatupa ni matokeo ya mtazamo wetu kuafikiana na mtazamo wake. Roho ya Mungu itatujaza mpaka tufurike ikiwa tutakuwa waangalifu ili kuendelea katika nuru. Hatuna udhuru kuwa wadhaifu katika nguvu ya Mungu.
Hatuna haki ya kumwambia Mungu kwamba hatuwezi kustahimili zaidi; Mungu anafaa kuwa huru kututendea atakavyo, kama alivyomtendea Mwana wake. Kisha chochote kitakachotendeka maishani mwetu yatajawa na furaha.
Maswali ya Kutafakari: Tabasamu yangu ni bandia ama ni ya kweli? Furaha yangu nia tumaini bandia ama mwanga wa kindani unaong'aa? Ninaamini kuwa Mungu atanipa furaha kupitia hali ambazo sichagui?
Dondoo imetoka "The Place of Help", © Discovery House Publishers

Andiko
Kuhusu Mpango huu
Gundua hekima ya Oswald Chambers, mwandishi wa "My Utmost for His Highest", katika mkusanyiko huu wa hazina ambao unatoa ufahamu kuhusu furaha. Kila somo lina dondoo kutoka Chambers na maswali ya kutafakari kibinafsi. Akitumia hekima sahili na dhahiri kutoka Biblia kukupa motisha na changamoto, utaanza kutamani kuwasiliana zaidi na Mungu.
More
We would like to thank Discovery House Publishers for providing this plan. For more information, please visit: www.utmost.org