Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Oswald Chambers: Furaha- Nguvu katika BwanaMfano

Oswald Chambers: Joy - Strength In The Lord

SIKU 26 YA 30

Dhambi, mateso, na utakaso si vitu dhahania pekee, bali ni ukweli wa maisha—mafumbo ambayo yanaamsha mafumbo mengine mpaka moyo unapotulia katika Mungu. Furaha ya kujua kwamba Mungu anatawala, kwamba yeye ni Baba yetu, kwamba mawingu ni “vumbi litimuliwalo na nyayo zake” haisemezeki! Maisha ya kidini yana msingi na hukomaa kwa sababu ya tumaini la dhati, yanabadilishwa na Upendo; kauli ya maisha hayo inatolewa na mtazamaji pekee, wala si mtakatifu.

Bwana, nimemlisha Kristo anayeishi ndani yangu kidogo sana; Ee Bwana, nisamehe. Nijaze na uwepo wa msamaha wako ili nisifurahi pekee katika ukombozi wako, bali pia nijazwe na Roho yako kwa ajili ya kazi yaliyoko huku.

Maswali ya kutafakari: Magumu, makosefu ya haki, na mafumbo ya maisha yananifanya nikate tamaa au yananishawishi kumtumainia Yeye anayenituma kuhubiri ujumbe kwamba upendo utashinda dhambi na mateso?

Dondoo imetoka "Christian Discipline" na "Knocking at God’s Door", © Discovery House Publishers

Andiko

siku 25siku 27

Kuhusu Mpango huu

Oswald Chambers: Joy - Strength In The Lord

Gundua hekima ya Oswald Chambers, mwandishi wa "My Utmost for His Highest", katika mkusanyiko huu wa hazina ambao unatoa ufahamu kuhusu furaha. Kila somo lina dondoo kutoka Chambers na maswali ya kutafakari kibinafsi. Akitumia hekima sahili na dhahiri kutoka Biblia kukupa motisha na changamoto, utaanza kutamani kuwasiliana zaidi na Mungu.

More

We would like to thank Discovery House Publishers for providing this plan. For more information, please visit: www.utmost.org