Oswald Chambers: Furaha- Nguvu katika BwanaMfano
Yesu si Mwokozi pekee, bali pia ni Mfalme, na ana haki ya kuchukua kitu chochote au vitu vyote ambavyo ni vyetu akitaka kufanya hivyo. Tunaongea kuhusu furaha na faraja ambao tunapata kwa wokovu; Yesu Kristu anaongea kuhusu kuchukua msalaba na kumfuata. Ni wachache sana ambao wanajua chochote kuhusu uaminifu kwake Yesu Kristu. Tunamwona Yesu Kristu kama Mfano mwema zaidi katika maisha ya Kikristo; lakini hatufikiri kwamba yeye ni Mwenyezi Mungu aliyekuja duniani, aliye na uwezo wote mbinguni na duniani. Tunamgeuza kuwa kama mwenzetu, Yeye ambaye katika vita hivi vya maisha ana pumzi kutushinda sote na anachukua muda wake kutusaidia. Tunahusiana naye kana kwamba Yeye ni kama sisi; hatuvui viatu vyetu anapozungumza. Yesu Kristu ni Mwokozi, na anatuokoa katika ubwana wake wa kweli na mtakatifu.
Maswali ya Kutafakari: Nimepata furaha ipi katika kujitolea? Ninafurahia zaidi Yesu kuwa mwenzako au Mfalme? Nina furaha zaidi nikifiri kutawala katika ufalme wa Mungu ama kuteseka ili ufalme wake uenee?
Dondoo inatoka "He Shall Glorify Me", © Discovery House Publishers
Maswali ya Kutafakari: Nimepata furaha ipi katika kujitolea? Ninafurahia zaidi Yesu kuwa mwenzako au Mfalme? Nina furaha zaidi nikifiri kutawala katika ufalme wa Mungu ama kuteseka ili ufalme wake uenee?
Dondoo inatoka "He Shall Glorify Me", © Discovery House Publishers
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Gundua hekima ya Oswald Chambers, mwandishi wa "My Utmost for His Highest", katika mkusanyiko huu wa hazina ambao unatoa ufahamu kuhusu furaha. Kila somo lina dondoo kutoka Chambers na maswali ya kutafakari kibinafsi. Akitumia hekima sahili na dhahiri kutoka Biblia kukupa motisha na changamoto, utaanza kutamani kuwasiliana zaidi na Mungu.
More
We would like to thank Discovery House Publishers for providing this plan. For more information, please visit: www.utmost.org