Oswald Chambers: Furaha- Nguvu katika BwanaMfano
Nafsi ambayo haina mahali pa upweke na Mungu imo hatarini kiroho. Je, tumeruhusu mahali haya ya upweke kuvunjwa ama madhabahu kujengwa juu yao ambayo yanapendeza kwa macho, na wapitanjia wanesama, “Kweli huyo mtu ni mcha Mungu.” Madhabahu ya aina hiyo ni tusi kwa kazi kuu ambayo Mungu anafanya rohoni mwetu. Mungu atujalie tujue zaidi na zaidi furaha kuu ya kuwa pekee yetu na Mungu usiku wa manane na inapoelekea kucha.
Katika kitabu cha Ufunuo, Yesu Kristu anajiita “wa kwanza na wa mwisho.” Ni katikati ambapo wanadamu wanafanya maamuzi; mwanzo na mwisho ni ya Mungu. Mungu anaamua kuzaliwa na kukufa, na kati ya mipaka hiyo mtu anajichagulia furaha ama huzuni.
Maswali ya Kutafakari: Ni wapi ambapo ni pahali pangu pa upweke na Mungu? Ninapenda kuwa na upweke na Mungu ama nina hamu kurudi kazini? Ninaanza kila siku kwa kuuliza Mungu nifanye nini na kumaliza kwa kumwuliza nilifanya aje?
Dondoo zimetoka "He Shall Glorify Me" na "Still Higher for His Highest", © Discovery House Publishers

Andiko
Kuhusu Mpango huu
Gundua hekima ya Oswald Chambers, mwandishi wa "My Utmost for His Highest", katika mkusanyiko huu wa hazina ambao unatoa ufahamu kuhusu furaha. Kila somo lina dondoo kutoka Chambers na maswali ya kutafakari kibinafsi. Akitumia hekima sahili na dhahiri kutoka Biblia kukupa motisha na changamoto, utaanza kutamani kuwasiliana zaidi na Mungu.
More
We would like to thank Discovery House Publishers for providing this plan. For more information, please visit: www.utmost.org