Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Oswald Chambers: Furaha- Nguvu katika BwanaMfano

Oswald Chambers: Joy - Strength In The Lord

SIKU 28 YA 30

Baraka za Mungu ni rahisi kuziona na kuzihisi mnamo wa maisha ya Kikristo, hadi Mkristo anaishi kwa kuona badala ya kwa imani, ni kama Mungu anamkumbatia. Lakini wakati unakuja ambao Mungu anaondoa faraja hizi, wakati ambao furaha katika Bwana si kama ilivyokuwa kitambo wakati ambao uwepo wake haupendezi kama awali, na ni kama kijivu kigeni (ikiwa tunaweza kusema hivyo) kinatanda juu ya maisha yetu ya kiroho.

Kwa muda, nafsi inaingia giza totoro; kisha inaanza kufahamu kwamba Mungu anaifunza tofauti kati ya kuishi katika mwanga wa baraka na kuhisi furaha ya kweli (ambayo Yesu aliongelelea katika hotuba yake mlimani); ama, kwa ufupi, Mungu anatoa nafsi kutoka kutegemea hisia na mihemko ya kidini na kuileta nafsi katika kuishi kwa imani.

Swali la Kutafakari: Mungu anatumia njia gani kunifunza kuishi kwa mwanga wa mbinguni wa furaha ya kweli badala ya mwanga bandia wa baraka za ulimwengu?

Dondoo linatoka "God’s Workmanship", © Discovery House Publishers

Andiko

siku 27siku 29

Kuhusu Mpango huu

Oswald Chambers: Joy - Strength In The Lord

Gundua hekima ya Oswald Chambers, mwandishi wa "My Utmost for His Highest", katika mkusanyiko huu wa hazina ambao unatoa ufahamu kuhusu furaha. Kila somo lina dondoo kutoka Chambers na maswali ya kutafakari kibinafsi. Akitumia hekima sahili na dhahiri kutoka Biblia kukupa motisha na changamoto, utaanza kutamani kuwasiliana zaidi na Mungu.

More

We would like to thank Discovery House Publishers for providing this plan. For more information, please visit: www.utmost.org