Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Oswald Chambers: Amani - Maisha kwenye RohoMfano

Oswald Chambers: Peace - Life in the Spirit

SIKU 21 YA 30

Baada ya Kuokoka mtu hupata amani, lakini ni amani endelevu katika hali ya vita. Tabia mbaya hainyanyuki, lakini bado ipo na mtu hujua ipo. Anafahamu jinsi ya kubadilisha, mda mwingine yupo kwenye furaha, mda mwiningine sio; hamna utulivu, hamna ushindi wa kiroho kiukweli. Kuchukua hali hiyo kama uzoefu wa wokovu kamili ni kumthibitisha kwamba Mungu hahusiki na upatanisho.

Kuwa mwamini wa Yesu Kristo inamaanisha kujua ambacho Yesu alimwambia Tomaso ni kweli: "Mimi ni njia, ukweli na uzima." Yesu sio barabara tunayoiacha ntunavyosafiri, lakini ni njia yenyewe. Kwa kuamini, tunaingia kwenye amani, utakatifu na uzima wa milele kwa sababu tunamfuata Yeye.

Maswali ya kutafakari: Ni amani ya aina gani tunapata kwa nguvu? Inachukua nini kudumisha amani ya aina hiyo? Kwanini makubaliano na Mungu ni muhimu kwa amani ya kweli?

Nukuu imetoka Biblical Ethics and Approved Unto God © Discovery House Publishers

Andiko

siku 20siku 22

Kuhusu Mpango huu

Oswald Chambers: Peace - Life in the Spirit

Amani: Maisha ya Roho ni hazina ya msukumo ya nukuu kutoka kwenye kazi za Oswald Chambers, mwandishi mpendwa ulimwenguni wa ibada na mwandishi wa My Utmost for His Highest. Pata mapumziko kwa Mungu na pata uelewa zaidi wa umuhimu wa amani ya Mungu kwenye maisha yako.

More

Tungependa kushukuru Huduma ya Discovery House Publishers kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.utmost.org