Zaburi 44:20-26
Zaburi 44:20-26 BHN
Tungalikuwa tumekusahau wewe Mungu wetu, tukamkimbilia mungu wa uongo, ee Mungu, ungalikwisha jua jambo hilo, kwa maana wewe wazijua siri za moyoni. Lakini kwa ajili yako twakikabili kifo kila siku; tunatendewa kama kondoo wanaopelekwa kuchinjwa. Amka, ee Bwana! Mbona umelala? Inuka! Tafadhali usitutupe milele! Mbona wajificha mbali nasi, na kusahau dhiki na mateso yetu? Tumedidimia hata mavumbini, tumegandamana na ardhi. Uinuke, uje kutusaidia! Utukomboe kwa sababu ya fadhili zako.