Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 44:20-26

Zaburi 44:20-26 SRUV

Ikiwa tumelisahau jina la Mungu wetu, Au kumnyoshea mungu mgeni mikono yetu; Je! Mungu hangegundua jambo hilo? Maana ndiye azijuaye siri za moyo. Hasha! Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa; Tunafanywa kama kondoo waendao kuchinjwa. Amka, Bwana, mbona umelala? Ondoka, usitutupe milele. Mbona unatuficha uso wako, Na kusahau kuonewa na kudhulumiwa kwetu? Maana nafsi yetu imeinama mavumbini, Tumbo letu limegandamana na nchi. Uinuke, uwe msaada wetu, Utukomboe kwa ajili ya fadhili zako.

Soma Zaburi 44