Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 44:20-26

Zab 44:20-26 SUV

Ikiwa tumelisahau jina la Mungu wetu, Au kumnyoshea mungu mgeni mikono yetu; Je! Mungu hatalichunguza neno hilo? Maana ndiye azijuaye siri za moyo. Hasha! Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa; Tunafanywa kondoo waendao kuchinjwa. Amka, Bwana, mbona umelala? Ondoka, usitutupe kabisa. Mbona unatuficha uso wako, Na kusahau kuonewa na kudhulumiwa kwetu? Maana nafsi yetu imeinama mavumbini, Tumbo letu limegandamana na nchi. Uondoke, uwe msaada wetu, Utukomboe kwa ajili ya fadhili zako.