Zaburi 44:20-26
Zaburi 44:20-26 NENO
Kama tungekuwa tumelisahau jina la Mungu wetu au kunyooshea mikono yetu kwa mungu mgeni, je, si Mungu angegundua hili, kwa kuwa anazijua siri za moyo? Hata hivyo kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa; tumehesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa. Amka, Ee Bwana! Kwa nini unalala? Zinduka! Usitukatae milele. Kwa nini unauficha uso wako na kusahau taabu na mateso yetu? Tumeshushwa hadi mavumbini, miili yetu imegandamana na ardhi. Inuka na utusaidie, utukomboe kwa sababu ya upendo wako usio na mwisho.