Maana kwenu yuko mtu anayetaka kujenga mnara, asiyekaa kwanza na kuzihesabu shilingi za jengo, kama anazo za kulitimiza? Kwani akiisha kuweka msingi, asipoweza kumaliza, halafu wote wanaoviona wataanza kumfyoza wakisema: Mtu huyu alianza kujenga, naye hakuweza kumaliza.