1
Luka 13:24
Swahili Roehl Bible 1937
Gombeeni, mpate kuuingia mlango ulio mfinyu! Nawaambiani: Wengi watataka kuuingia, lakini hawataweza.
Linganisha
Chunguza Luka 13:24
2
Luka 13:11-12
Mle nyumbani mkawa na mwanamke mwenye pepo aliyemwuguza miaka 18; kwa hiyo alikuwa amepindana, asiweze kunyoka kamwe. Yesu alipomwona akamwita, akamwambia: Mama, umefunguliwa huu unyonge wako
Chunguza Luka 13:11-12
3
Luka 13:13
Kisha akambandikia mikono yake. Papo hapo akanyoka, akamtukuza Mungu.
Chunguza Luka 13:13
4
Luka 13:30
Tazameni, wako wa mwisho watakaokuwa wa kwanza, tena wako wa kwanza watakaokuwa wa mwisho.
Chunguza Luka 13:30
5
Luka 13:25
Tangu hapo, mwenye nyumba atakapoinuka na kuufunga mlango, ndipo, mtakapoanza kusimama nje na kuugonga mlango mkisema: Bwana, Bwana, tufungulie! Naye atajibu akiwaambia: Siwajui ninyi, mtokako.
Chunguza Luka 13:25
6
Luka 13:5
Nawaambiani: Sivyo, ila msipojuta nyote mtaangamia vivyo hivyo.
Chunguza Luka 13:5
7
Luka 13:27
Ndipo, atakapowaambia ninyi: Siwajui, mtokako, ondokeni kwangu nyote mfanyao mapotovu!
Chunguza Luka 13:27
8
Luka 13:18-19
Kisha akasema: Ufalme wa Mungu umefanana na nini? Niufananishe na nini? Umefanana na kipunje cha haradali, alichokitwaa mtu na kukitupia shambani kwake. Nacho hukua na kupata kuwa mti, hata ndege wa angani hutua katika matawi yake.
Chunguza Luka 13:18-19
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video