1
Ufunuo 2:4
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Lakini nina neno dhidi yako: Umeuacha upendo wako wa kwanza.
Linganisha
Chunguza Ufunuo 2:4
2
Ufunuo 2:5
Kumbuka basi ni wapi ulikoanguka! Tubu na ukafanye matendo yale ya kwanza. Kama usipotubu, nitakuja kwako na kukiondoa kinara chako cha taa kutoka mahali pake.
Chunguza Ufunuo 2:5
3
Ufunuo 2:10
Usiogope mateso yatakayokupata. Nakuambia ibilisi atawatia baadhi yenu gerezani ili kuwajaribu, nanyi mtapata dhiki kwa muda wa siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji la uzima.
Chunguza Ufunuo 2:10
4
Ufunuo 2:7
Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho wa Mungu ayaambia makundi ya waumini. Yeye ashindaye, nitampa haki ya kula matunda ya uzima, ambao uko katika paradiso ya Mungu.
Chunguza Ufunuo 2:7
5
Ufunuo 2:2
Nayajua matendo yako, bidii yako na saburi yako. Najua kuwa huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewajaribu wale wanaojifanya mitume na kumbe sio, nawe umewatambua kuwa ni waongo.
Chunguza Ufunuo 2:2
6
Ufunuo 2:3
Umevumilia na kustahimili taabu kwa ajili ya Jina langu, wala hukuchoka.
Chunguza Ufunuo 2:3
7
Ufunuo 2:17
Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho wa Mungu ayaambia makundi ya waumini. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa. Nitampa pia jiwe jeupe ambalo juu yake limeandikwa jina jipya asilolijua mtu, isipokuwa yule anayelipokea.
Chunguza Ufunuo 2:17
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video