Kama vile mvua na theluji
ishukavyo kutoka mbinguni,
nayo hairudi tena huko
bila kunywesha dunia
na kuichipusha na kuistawisha,
ili itoe mbegu kwa mpanzi
na mkate kwa mlaji,
ndivyo lilivyo neno langu litokalo kinywani mwangu:
Halitanirudia tupu,
bali litatimiliza lile nililokusudia,
na litafanikiwa katika kusudi lile nililolituma.