YouVersion Logo
Search Icon

Plan Info

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023Sample

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023

DAY 6 OF 31

Je, wewe unataka kufanya mapenzi ya Mungu? Unajua ni nini hasa? Yesu anasema ndiyo kumwamini aliyetumwa na Mungu (m.29,Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye). Kumwamini Yesu ni sawa na sisi kwenda kwake kwa njia ya maombi na kula chakula chake. Yesu anatusihi tusikishughulikie chakula cha mwili tu, bali hasa hicho kitokacho mbinguni na kumpa kila anayekila uzima wa milele. Mwenyewe ndiye chakula hicho. Anasema,Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe(m.35). Tukimwamini Yesu atatushughulikia katika yote. Hatutaona njaa ya kiroho na siku ya mwisho atatufufua kimwili ili tuwe kwake milele.

Scripture

Day 5Day 7

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu Yohana na Mithal...

More

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy