YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 12/2020Sample

Soma Biblia Kila Siku 12/2020

DAY 8 OF 31

Neno la leo ni mwendelezo wa mafundisho ya hali itakavyokuwa siku za mwisho. Hata maeneo ya ibada yatashambuliwa au kuchafuliwa. Dhiki na mateso ya kutisha yatashamiri na uzushi wa kurudi kwa masihi utasikika. Manabii na wakristo wa uwongo watainuka na kupotosha wengi. Lakini, Mungu ashukuriwe! Ameikatisha dhiki ili wateule wake waokoke. Na Yesu ameyabainisha haya kwa sababu ya upendo ili tusiwe gizani. Tafakari matukio yote kwa uelewa utakaokufanya ukeshe kumngoja Bwana atakaporudi.

Day 7Day 9

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 12/2020

Soma Biblia Kila Siku 12/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wathesalonike, Mathayo na Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More