YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 12/2020Sample

Soma Biblia Kila Siku 12/2020

DAY 9 OF 31

Kurudi kwa Bwana Yesu kutatanguliwa na ishara ya wazi. Na hatimaye atakapoonekana, vilio vya huzuni kwa waliombeza vitaijaza anga. Hoi hoi za furaha zitasikika kwa waliomwamini. Ni siku ya ajabu wateule watakapokuwa wanakusanywa mbele ya Mfalme Yesu kwa mashangilio makuu. Bwana atuonya tusome sana matukio ya ulimwenguni. Ndiyo yanayotuandaa kuelewa bila mashaka kwamba Mwana wa Mungu yu karibu mlangoni. Nayo yatutosha kujiandaa kumlaki Bwana Yesu badala ya kudadisi tarehe ya tukio hilo; ambayo Mungu ameiweka sirini mwake.

Day 8Day 10

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 12/2020

Soma Biblia Kila Siku 12/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wathesalonike, Mathayo na Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More