YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 12/2020Sample

Soma Biblia Kila Siku 12/2020

DAY 11 OF 31

Yesu analinganisha kurudi kwake na mwizi anavyoingia katika nyumba. Mwizi huingia kwa mtu saa asiyojua na hutenda uharibifu wa kusikitisha. Kwa Wakristo wote, hiki ni kielelezo kizuri kuonyesha inavyotupasa kukesha tukimngoja Bwana wetu. Kuna hatari ya sisi kukutwa tumelala arudipo Bwana wetu. Epuka hasara ya kukutwa umelala na Bwana wako. Fanya kama walinzi wafanyavyo: wao wanajua kuwa kukaa macho, kusikiliza na kuchunguza kila tendo lenye mashaka maishani ndiyo njia ya kujiepusha na hasara. 

Day 10Day 12

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 12/2020

Soma Biblia Kila Siku 12/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wathesalonike, Mathayo na Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More