YouVersion Logo
Search Icon

Plan Info

Soma Biblia Kila Siku 12/2020Sample

Soma Biblia Kila Siku 12/2020

DAY 7 OF 31

Hekalu ilikuwa fahari ya Wayahudi. Liliashiria uhusiano wao na Mungu, na ndani yake walionana na Mungu. Wanafunzi walilionea shauku. Lakini Yesu alitabiri kuwa siku moja lingebomolewa; na lilibomolewa mwaka 70 b.K. Pia Bwana alitumia nafasi hii kueleza dalili za nyakati za mwisho. Je umegundua dalili kuu na ndogo za kurudi kwa Yesu mara ya pili katika somo la leo? Tunaposoma na kuona dhahiri dalili hizi zinapotimia, hatuna budi kujiandaa kwa kudumu ndani ya imani katika Yesu Kristo (Yn 15:5-7, Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea.Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa). 

Day 6Day 8

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 12/2020

Soma Biblia Kila Siku 12/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wathesalonike, Mathayo na Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mun...

More

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy