YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 8Sample

Soma Biblia Kila Siku 8

DAY 3 OF 31

Paulo alijieleza kwa Wayahudi kuhusu sababu ya yeye kuwepo huko. Alifikiri huenda wameisikia habari yake na kutaka kumwua. Lakini walikuwa hawajasikia lolote, na walikuwa tayari kumsikiliza (m.21-22: Wakamwambia, Sisi hatukupata nyaraka zenye habari zako kutoka Uyahudi, wala hapana ndugu hata mmoja aliyefika hapa na kutupasha habari, au kunena neno baya juu yako.
Lakini tunataka kusikia kwako uonavyo wewe; kwa maana katika habari za madhehebu hiyo imejulikana kwetu kwamba inanenwa vibaya kila mahali). Hatusikii zaidi kuhusu kesi yake Paulo. Ila tunaona kwamba kwa miaka miwili hii alipokaa Rumi alikuwa na uhuru kiasi kikubwa. Muda wote alitumia kwa ajili ya kufundisha watu neno la Mungu (m.30-31:Akakaa muda wa miaka miwili mizima katika nyumba yake aliyokuwa ameipanga, akawakaribisha watu wote waliokuwa wakimwendea, akihubiri habari za ufalme wa Mungu, na kuyafundisha mambo ya Bwana Yesu Kristo, kwa ujasiri mwingi, asikatazwe na mtu). Baadaye alifunguliwa (tunavyojua ilitokea mwaka 62 BK) na kufanya tena safari ya misioni. Mwisho akauawa na Kaisari Nero huko Rumi mwaka 64 BK.

Scripture

Day 2Day 4