Soma Biblia Kila Siku 8Sample
Katika somo hili twaona upendo mkuu alio nao Yesu kwa wanafunzi wake. Aliwaona jinsi walivyohangaika. Akaja kuwasaidia. Akawapikia chakula. Wakala pamoja. Hivyo akawahakikishia tena kuwa yu hai na hajawaacha. Pia twatambua jambo lingine muhimu: Yesu siye roho tu. Alifufuka kimwili! Ni roho na mwili. Maana alikula chakula! (m.13: Yesu akaenda akautwaa mkate, akawapa, na samaki vivyo hivyo.) Na alama za majeraha alikuwa nazo mwilini! (Yn 20:27-28: Yesu akamwambia Tomaso, Lete hapa kidole chako; uitazame mikono yangu; ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu, wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye. Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu!Hata Mbinguni anazo. Yohana anashuhudia: Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa(Ufu 5:6).) Hivi atatufufua na sisi tukiwa na mwili wa utukufu (Flp 3:20-21: Sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo; atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake)!
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 8 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku hasa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Kumbukumbu la Torati, na Yohana pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More